KazaVPN ya Android TV
Tumia programu za TV yako bila mtoa huduma wako wa intaneti kuona ni zipi, kwa rimoti peke yake.
Inakuja hivi karibuni kwa Android
Fungua akaunti yako ya bure sasa na uingie siku itakapowasili.
Inachofanya kwenye TV yako
Imeundwa kwa ajili ya rimoti
Kila skrini inafanya kazi kwa vitufe vya mishale na kitufe cha kuchagua. Huhitaji kipanya, kibodi wala simu.
Tazama kutoka nchi nyingine
Ukiwa na KazaVPN Premium, chagua nchi, na programu za TV yako zinaona anwani ya huko.
Acha baadhi ya programu nje
Chagua programu za TV zinazopitia KazaVPN, na uache nyingine zitumie muunganisho wa nyumbani kama kawaida.
Iweke kwa kutumia rimoti
Weka faili kwenye TV
Pakua faili ya Android kutoka ukurasa huu kwenye kivinjari cha TV, au inakili kwenye TV kutoka kwenye flash ya USB.
Isakinishe
Fungua faili kwenye kidhibiti faili cha TV. Android TV ikiuliza, iruhusu programu hiyo kusakinisha programu zisizojulikana, kisha chagua “Sakinisha”.
Ingia kwa rimoti
Fungua KazaVPN kutoka kwenye programu za TV yako. Nambari ya akaunti ndiyo rahisi zaidi kuandika kwa rimoti.
Unachohitaji
- Android 9 au toleo jipya zaidi
- TV au kisanduku cha kutiririsha chenye Android TV au Google TV.
- Flash ya USB au kivinjari cha TV yenyewe, ili kuweka programu ndani yake.
Maswali kuhusu KazaVPN kwenye TV
Je, programu zangu za kutiririsha zitacheza kupitia KazaVPN?
Kila huduma inaamua hilo yenyewe. KazaVPN inaipa TV yako anwani katika nchi unayochagua; kama huduma inacheza huko ni uamuzi wa huduma hiyo, si wetu.
TV yangu haina Android TV. Bado inaweza kulindwa?
Ndiyo, kupitia ruta yako. Weka KazaVPN kwenye ruta mara moja, na kila kitu kilichounganishwa nayo kinalindwa, ikiwemo TV janja na koni ya michezo.
Je, TV inahesabiwa kama mojawapo ya vifaa vyangu?
Ndiyo, TV iliyoingia kwenye KazaVPN inahesabiwa kama simu. Ondoa kifaa usichotumia tena kwenye ukurasa wa akaunti yako ili kuachia nafasi yake.
TV inasema programu haioani nayo. Nifanye nini sasa?
Baadhi ya TV zinahitaji faili ya vifaa vya zamani. Chukua ile ya 32-bit ARM kutoka “Vipakuliwa vyote vya Android” na uisakinishe badala yake.
