Sakinisha KazaVPN kwenye Android

Unasakinisha programu ya Android moja kwa moja kutoka ukurasa wetu wa kupakua. Inachukua dakika chache, na Android inakuomba ruhusa mara moja tu.

Chagua faili yako

Ukurasa wa kupakua una kitufe kimoja kwa kila aina ya kifaa. Simu na kompyuta kibao nyingi zinahitaji kitufe cha kwanza.

Android ikisema programu hii haioani na kifaa chako, tumia kitufe cha pili, ambacho ni cha simu za zamani. Cha tatu ni cha kompyuta inayoendesha Android. Chromebook itapata KazaVPN kutoka Google Play mara itakapoorodheshwa huko, hivi karibuni.

Ipakue

Tumia kivinjari kwenye simu au kompyuta kibao unayotaka kutumia KazaVPN.

  1. Fungua ukurasa wa kupakua na uguse kitufe cha kifaa chako.
  2. Kivinjari kikisema huenda faili hii ikadhuru na kuuliza kama uipakue hata hivyo, gusa “Pakua hata hivyo”.
  3. Upakuaji ukikamilika, gusa “Fungua”. Unaweza pia kupata faili baadaye katika Vipakuliwa vyako.

Ruhusu usakinishaji na ufungue KazaVPN

Android inauliza mara moja kabla ya kusakinisha programu uliyopakua kwa kivinjari.

  1. Android ikisema simu yako hairuhusiwi kusakinisha programu zisizojulikana kutoka chanzo hiki, gusa “Mipangilio”.
  2. Washa “Ruhusu kutoka kwenye chanzo hiki”, kisha urudi nyuma.
  3. Gusa “Sakinisha”. Google Play Protect ikiomba kuchanganua programu kwanza, gusa “Changanua programu”.
  4. Gusa “Fungua” na uingie kwa akaunti yako ya KazaVPN.

Unaweza kuzima “Ruhusu kutoka kwenye chanzo hiki” tena baadaye. Android itaiomba tena pale tu utakaposakinisha sasisho kwa njia hiyo hiyo.

Kagua faili

Hatua hii ni ya hiari. Ukurasa wa kupakua unaonyesha alama ya kidole ya kila faili chini ya “Kagua faili”: msimbo mrefu unaobadilika kabisa hata herufi moja tu ya faili ikitofautiana. Android yenyewe inakataa faili iliyoharibika. Ili kulinganisha pia alama ya kidole, pakua faili kwenye kompyuta na uendeshe amri ya kompyuta hiyo iliyo hapa chini.

Windows

Get-FileHash $HOME\Downloads\kazavpn-android-*.apk

Mac

shasum -a 256 ~/Downloads/kazavpn-android-*.apk

Linux

sha256sum "$(xdg-user-dir DOWNLOAD)"/kazavpn-android-*.apk

Msimbo unaoonyeshwa ukilingana na alama ya kidole iliyo kwenye ukurasa wa kupakua, nakili faili kwenye simu yako na uisakinishe kutoka hapo. Isipolingana, futa faili na uipakue tena.

Kusasisha KazaVPN

Toleo jipya likitoka, KazaVPN itakujulisha. Pakua faili mpya kutoka ukurasa wa kupakua na uisakinishe kwa njia ile ile. Inachukua nafasi ya toleo la zamani na unabaki umeingia.

Pata msaada kutoka kwa timu yetu

Wanachama wa KazaVPN Premium na KazaVPN Family wanapata majibu kutoka kwa mtu wa timu yetu, kwa barua pepe.

Akaunti moja kwenye kila kifaa ulicho nacho